Sunday 11 May 2014

Waganga wa Jadi watahadharishwa kutumia Alama ya Msalaba Mwekundu

Na Stephano Simbeye,

Chama Cha Msalaba mwekundu kimewatahadharisha waganga wa jadi pamoja na taasisi zingine zinazotumia Alama ya msalaba Mwekundu katika shughuli zao kuwa ni makosa na ni kinyume na sheria.

Tahadhari hii ilitolewa na Makamu wa raisi wa chama hicho Dr. Zainabu Gama alipokuwa akihutubia katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya msalaba mwekundu duniani zilizofanyikia kitaifa mkoani mbeya katika viwanja vya Rwanda Nzovwe.

Dr. Zainabu alisema kuwa kumekuwa na matumizi holela ya alama ya Msalaba mwekundu ambapo nembo hiyo inatumiwa na baadhi ya waganga wa jadi katika shughuli zao ikiwamo na baadi ya taasisi zingine amabazo hazina uhusiano kabisa na chama cha msalaba mwekundu.
Aliziweka wazi taasisi zingine zinazotumia alama hiyo kimakosa kuwa ni pamoja na hospitari na magari ya kubebea wagonjwa.
                                  
Alama ya msalaba inayotumiwa na Chama Cha Msalaba Mwekundu (picha kutoka mtandaoni)

Dr. Zainabu alitoa msisitizo kuwa matumizi holela ya nembo hiyo ni kinyume na sheria ya mwaka 1962 iliyoundwa na chama cha msalaba mwekundu ambayo kwa sasa inafanyiwa marekebisho na bunge inayoruhusu alama ya msalaba mwekundu kutumiwa na chama cha msalaba mwekundu na sehemu ya jeshi  tu ambayo ndiyo inayotoa huduma za kiafya katika chama hicho.

“Naiomba serikari kuchukua hatua za haraka kurekebisha sheria ya msalaba mwekundu ili kuweza kudhibiti matumizi holela ya nembo hiyo” alisema Dr. Zainabu

Kwa upande wake mgeni rasmi wa sherehe hizo kutoka Wizara ya Afya Bw. Deodatus Kinawilo alidhibitisha kutumika kwa alama ya msalaba mwekundu katika shughuli za hospitali za serikali pamoja na magari ya kubebea wagonjwa na aliahidi kutafuta namna ya kuweza kalitatua swala hilo.

Aidha Dr. Zainabu alitoa ufafanuzu juu ya utofauti uliopo kati ya alama ya msalaba inayotumiwa na chama cha msalaba mwekundu na ile inayotumiwa makanisani kuwa  alama ya msalaba inayotumiwa na chama cha msalaba mwekundu ina nguo mbili zenye urefu sawa wakati nembo inayotumiwa makanisani ina nguzo msimamo ambayo ni ndefu zaidi ya nguzo mlalo.

Alama ya Msalaba inayotumiwa Makanisani (picha toka mtandaoni)

Sunday 27 April 2014

Wahanga wa mafuriko kyela wahitaji msaada wa hari na mari

    Kutokana na mafuriko makubwa yaliyotokea hivi karibuni wilayani kyela, wakazi wengi wamejikuta hawana uhakika wa kujipatia chakula, mahala pa kulala, Mavazi ya kuvaa wala uhakika kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi na Kupelekea hali kuwa tete zaidi.
  waathirika wakubwa wa adha hizi ni kundi la watoto na wanawake.
     

baadhi ya wanachi waliokosa makazi baaada  ya makazi yao kuingiliwa na mafuriko

wananchi wenye mapenzi mema na moyo wa huruma wanaombwa kujitolea kuwasaidia wahanga hawa kwa chochote, kama Vyakula, Mavazi na fedha.
       kwa upande wa mkoa wa mbeya shughuli za ukusanyaji wa misaada kwa ajiri ya wahanga hawa zinaendeshwa na Taasisi ya Muungano wa Jamii Tanzania (MUJTA) ikishirikiana na Red Cross na skauti.


         wanachi wakivuka moja  ya madalaja ya mto kiwira yaliyojaa maji kutokana na mto huo kufurika.


zoezi la ukusanyaji wa misaada hii litaanza tarehe 28 / 05 / 2014. na wakusanyaji watapita maeneo mbali mbali wakiwa wamevalia mavazi ya red cros, Mashat ya MUJATA ama watakuwa na vitambulisho vya mujata.
watanzania mnaombwa ushirikano wenu ili kuweza kuwakwamua ndugu zetu hawa kama ilivyo desturi yetu watanzania ya kupendana na kusaidiana


      baadhi ya maeneo ya makazi ya watu yaliyoingiliwa na maji

vituo maalum vya ukusanyaji wa misaada hiyo vitatajwa kupaitia redia zote za mbeya ama kupitia blog hii. na namba za simu kwa ajiri ya kutuma pesa zitatajwa pia redioni humo


maeneo mengine ya barabara na mashamba yaliyokumbwa na mafuriko wilayani kyela