Na Stephano Simbeye,
Chama Cha Msalaba mwekundu kimewatahadharisha waganga wa
jadi pamoja na taasisi zingine zinazotumia Alama ya msalaba Mwekundu katika
shughuli zao kuwa ni makosa na ni kinyume na sheria.
Tahadhari hii ilitolewa na Makamu wa raisi wa chama hicho
Dr. Zainabu Gama alipokuwa akihutubia katika kilele cha sherehe za maadhimisho
ya siku ya msalaba mwekundu duniani zilizofanyikia kitaifa mkoani mbeya katika
viwanja vya Rwanda Nzovwe.
Dr. Zainabu alisema kuwa kumekuwa na matumizi holela ya
alama ya Msalaba mwekundu ambapo nembo hiyo inatumiwa na baadhi ya waganga wa
jadi katika shughuli zao ikiwamo na baadi ya taasisi zingine amabazo hazina
uhusiano kabisa na chama cha msalaba mwekundu.
Aliziweka wazi taasisi zingine zinazotumia alama hiyo
kimakosa kuwa ni pamoja na hospitari na magari ya kubebea wagonjwa.
Alama ya msalaba inayotumiwa na Chama Cha Msalaba Mwekundu (picha kutoka mtandaoni)
Dr. Zainabu alitoa msisitizo kuwa matumizi holela ya nembo
hiyo ni kinyume na sheria ya mwaka 1962 iliyoundwa na chama cha msalaba mwekundu
ambayo kwa sasa inafanyiwa marekebisho na bunge inayoruhusu alama ya msalaba
mwekundu kutumiwa na chama cha msalaba mwekundu na sehemu ya jeshi tu ambayo ndiyo inayotoa huduma za kiafya
katika chama hicho.
“Naiomba serikari kuchukua hatua za haraka kurekebisha
sheria ya msalaba mwekundu ili kuweza kudhibiti matumizi holela ya nembo hiyo”
alisema Dr. Zainabu
Kwa upande wake mgeni rasmi wa sherehe hizo kutoka Wizara ya
Afya Bw. Deodatus Kinawilo alidhibitisha kutumika kwa alama ya msalaba mwekundu
katika shughuli za hospitali za serikali pamoja na magari ya kubebea wagonjwa
na aliahidi kutafuta namna ya kuweza kalitatua swala hilo.
Aidha Dr. Zainabu alitoa ufafanuzu juu ya utofauti uliopo kati
ya alama ya msalaba inayotumiwa na chama cha msalaba mwekundu na ile
inayotumiwa makanisani kuwa alama ya
msalaba inayotumiwa na chama cha msalaba mwekundu ina nguo mbili zenye urefu
sawa wakati nembo inayotumiwa makanisani ina nguzo msimamo ambayo ni ndefu zaidi
ya nguzo mlalo.
Alama ya Msalaba inayotumiwa Makanisani (picha toka mtandaoni)